Kila Sherehe Ina Hadithi. Tuianze kwa Mwaliko wa Kipekee.
Karibisha wageni kwa mialiko ya kidijitali yenye mvuto, iliyobuniwa kwa harusi, send-off, kitchen party, siku za kuzaliwa na hafla nyingine.
Ulizia HudumaFahamu Huduma ZetuSherehe Yako, Mtindo Wako
Chagua aina ya sherehe yako na ujionee miundo inayoweza kukuvutia.
Huduma Zetu
Kuanzia mialiko ya WhatsApp na SMS hadi uthibitisho wa mahudhurio na uhakiki wa wageni, tunalenga kukusaidia kuwasiliana kwa urahisi.
Mialiko kwa SMS
Wafikishie wageni taarifa muhimu za sherehe kupitia ujumbe mfupi wa simu, hata bila kutumia intaneti.
Uthibitisho wa Mahudhurio (RSVP)
Pata majibu ya wageni kuhusu kuhudhuria ili uweze kupanga sherehe yako kwa utulivu.
Mialiko Yenye Majina ya Wageni
Mpe kila mgeni mwaliko unaomtaja kwa jina na kuonyesha taarifa zinazomhusu.
Mialiko Yenye QR Code
Rahisisha uhakiki wa mialiko na mapokezi ya wageni siku ya tukio.
Ufuatiliaji wa Mahudhurio
Fahamu idadi ya wageni waliothibitisha na waliofika ili kurahisisha maandalizi.
Vikumbusho kwa SMS
Kukumbusha wageni kuhusu tarehe, muda na mahali pa sherehe, pamoja na kutoa/kukamilisha ahadi na michango kwa ujumbe mfupi.
Baadhi ya Kazi Zetu
Kila sherehe ina mtindo wake. Tazama baadhi ya miundo ya mialiko yetu.
